Maswa: Ukosefu wa miundombinu bora katika Stund ya bus halmashauri ni chanzo.
6 May 2023, 8:32 am
Na Alex.F.Sayi
UMOJA wa Mawakala wa Usafirishaji Stund Mpya iliyopo wilayani Maswa Mkoani Simiyu wameulalamikia uongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa ubovu wa miundombinu katika stund hiyo licha ya kutozwa ushuru kwa kila gari inayoingia hapo.
Akizungumza na Sibuka Fm akiwa katika eneo la Stund hiyo wakati wa kufanya usafi Mwenyekiti wa Umoja huo Hassan Bunango amesema kuwa licha ya mazungumzo ya muda mrefu na Halmashauri hiyo hawaoni chochote kinachofanyika kuboresha Stand hiyo.
“Hii kero imekuwa ya muda mrefu sana tumelizungumzia sana hili jambo lakini hatuoni kinachoendelea,Stand hii miundombinu yake mibovu,Stand nichafu ona nyasi zilivyondefu bado njia yakuingilia magari mbovu,ukienda Chooni hovyoo.”Alisema Bunango
Bunango ameongeza kuwa Halmashauri hiyo inalipisha ushuru wa Sh.3,000 kwa kila Gari lakini hawaoni mapato hayo yanafanya nini kwenye Stund hiyo ambapo walikubaliana waweke molamu lakini mpaka sasa hawajaweka eneo limejaa Nyasi tu limebaki lakuchungia Mifugo katika Stund hiyo.
“Ukifanya hesabu ya kawaida magari yanayoingia hapa ni 70 kwa kila ambapo kila gari hulipia ushuru wa Sh.3000 kwa siku ni Sh. 210,000 kwa mwaka nizaidi ya Sh.Mill 75 hayo ni magari tu lakini kuna vibanda hapa vinalipia ushuru Halmashauri hizi hela zinafanya kazi gani.”Amesema Mwenyekiti huyo.
Abrazack Msuya ,Mwenyekiti Kitongoji cha Stund Mpya amesema kuwa wamelazimika kusema na umoja wa wasafirishaji na wafanyabiasha wa Stund hiyo ili wajitolee kufyeka Nyasi na kufanya usafi wa eneo hilo,ili Stund hiyo iwe kwenye hali ya usafi.
“Siku zote natumia mfumo wa Ulaghibishi kwenye Kitongaji changu nawashirikisha wadau waone umuhimu wa kuwajibika badala yakulalamika nakuisubiria Serikali kama unavyoona hapa tunaendelea na kazi tunatimiza wajibu wetu ili Serikali nayo ije ifanye kwa sehemu yake.”Amesema Msuya.
Prisca Sebastiani, ni mmoja wa Wasafirishaji hao ameuomba uongozi wa Halmashauri hiyo utumie nusu ya fedha hizo kuwapatia TASAF ili usaidie kufanya usafi kwenye eneo hilo ,huku akilalamikia huduma ya Choo kutokuwa na mfumo wa Maji Tiririka hali inayopelekea mazingira ya Choo hicho kuwa machafu.
Budodi Walwa,ni afisa afya Wilaya ya Maswa amesema kuwa uwepo wa nyasi hizo unatokana na wamiliki wa vibanda kushindwa kufanya usafi kwenye maeneo yao kama utaratibu unavyoelekeza.
“Halmashauri imeajiri watu wawili kufagia na kufyeka eneo la wazi na unajua Stund hiyo ipo chini ya Mamlaka ya Mji mdogo inalisimamia eneo hilo na tunafanya hivyo ila eneo linalobaki la vibanda kama wamiliki wa vibanda wangefanya usafi Stund ingekuwa Safi.”Amesema Walwa.
Akizungumzia suala hilo Simon Nyadwera, Mtendaji Mamla ya Mji Mdogo Maswa amesema kuwa suala la Usafi ni wajibu wa kila Mtanzani hivyo hakuna sababu ya mtu kulalamika kwa kisingizio cha kulipa ushuru.
“Tunachojua sisi nikwamba Stund ile bado ipo kwenye maboresho haijakamirika na ndoo maana vibanda vingi havina watu na maeneo hayo ndoo unaona kunanyasi nyingi,sisi tunawatu wanaofanya usafi hapo tatizo eneo nikubwa na kama kunawatu wamejitolea kufanya usafi ni jambo jema kikubwa tushirikishane.”Amesema Nyadwera.