Father Mashenene atoa Msaada wa Baiskeli za walemavu S/Msingi Malampaka.
15 April 2023, 8:10 pm
Baba Paroko wa Parokia ya Malampaka Jimbo la Shinyanga Padre Renatus Mashenene ametoa msaada wa Baiskeli mbili za Walemavu kwa shule ya Msingi Malampaka iliyopo Wilayani Maswa Mkoani Simiyu ili kuunga mkono Jitihada za Serikali ya awamu ya sita ya kuwajali watu wenye Makundi maalumu.
Baba Paroko Mashenene amesema kuwa watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine hivyo wana haki za kupata mahitaji yote ya Muhimu ya Binadamu huku akielezea kuwa sisi Binadamu wote ni ndugu tunapaswa kupendana na kuondoa Ubinafsi kati yetu.
Sauti ya Father Mashenene..
Amesema kuwa wakati mwingine Mungu huruhusu kila mmoja Kuzaliwa Jinsi alivyo ili tu Mapendo yake yatimie kwani kila mmoja ana thamani mbele za Mungu iwe Masikini au Tajiri, Mwembamba au mnene, mdogo au mkubwa.
Sauti ya Father Mashenene
Akipokea Baiskeli hizo kutoka kwa Father Mashenene, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe, Aswege Kaminyoge amemshukuru Father Mashenene kwa msaada huo ambao unaenda kutimiza Azima ya Serikali ya kuwapatia Mahitaji Muhimu watu wenye Ulemavu hivyo wadau wengine Waige Mfano huo.
Sauti ya DC Maswa Kaminyoge
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Saimon Berege amesema kuwa Jambo ambalo amefaya Father Mashenene linaleta Baraka mbele za Mwenyezi Mungu a kumsihi asichoke kusaidia kwani uhitaji kwa watu wenye Ulemavu ni mkubwa.
Sauti ya DED Maswa Saimon Berege
Akitoa Taarifa kwa Mkuu wa wilaya, Afisa Elimu, Elimu maalumu wilaya hapa Abel Charahani Lucas amesema kuwa Jumla ya watoto 182 wenye Ulemavu mbalimbali katika wilaya ya Maswa ambao wapo shuleni wanaendelea na Masomo..
Sauti ya Abel Charahani Afisa Elimu, Elimu Maalumu Maswa
Josephina Clementi ni Mama Mzazi wa mtoto mwenye Ulemavu amemshukuru Father Mashenene kwa Msaada wa Baiskeli hiyo ambayo itamsaidia mwanae kwenda shule kila siku
Sauti ya Josephina Clementi mama mwenye mtoto Mlemavu.
Hapa chini picha za Matukio ya Hafla ya kukabidhi Msaada wa Baiskeli kwa Wanafunzi wenye Ulemavu shule ya Msingi Malampka.