Waziri Mkuu Majaliwa aonya Matumizi ya Fedha mbichi kwenye Halmashauri
25 March 2023, 9:26 pm
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Kasimu Majaliwa amezionya Halmashauri zinazotumia Fedha za Makusanyo ya ndani kabla ya kuziweka kwenye Mifumo ya Kibenki.
Mhe Majaliwa ametoa Onyo hilo leo mjini Bariadi wakati akiongea na baadhi ya Watumishi wa Mkoa wa Simiyu Baada ya kuzindua Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Bariadi Mji.
Amesema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya Halmashauri kukusanya Fedha za Mapato na kuzipangia Matumizi kabla ya kuziingiza kwenye Benki ili zionekane kwenye Mifumo ya kifedha ya Serikali.
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa amemuonya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega kwa kupuuza maagizo ya Mh Rais Dkt Samia Suluhu Hasani ya kujenga Soko mji wa Lamadi na badala yake yeye kuamua kujenga Nyashimo.
Akitoa Salama za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda amemshukuru Rais Samia kwa Fedha nyingi alizoleta kwa ajili ya Shughuli za Maendeleo..
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Simiyu Ndugu Shamsa Mohamed amesema kuwa kumekuwepo na baadhi ya Viongozi wa ngazi za juu kuwatishia watumishi wa ngazi ya chini.