Bilioni 4.2 Kutengeneza na Kukarabati Barabara wilayani Maswa
1 February 2023, 2:38 pm
Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini ( TARURA) Wilayani Maswa Mkoani Simiyu imepanga kutumia Zaidi ya Tsh, Bilioni 4.22 kwa mwaka wa Fedha 2023/ 2024 katika Kukarabati na Kutengeneza Mtandao wa Barabara..
Akiwasilisha Taarifa ya Makadirio hayo ya Fedha kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani, Kaimu Meneja Tarura Wilayani hapa Mhandisi Francis Kuya amesema kuwa Bajeti hiyo imezingatia Vipao mbele vilivyoibuliwa na Wananchi na Hali ya Upitikaji.
Katika Bajeti Mhandisi Kuya amesema kuwa Fedha hizo zinatokana na Mfuko wa Barabara, Mfuko wa Jimbo na Pamoja na Tozo za Mafuta kama anavyoeleza.
Nao Baadhi ya Madiwani (Bundala Isambaja Kata ya Nyalikungu na Aroni Mboje Diwani wa kata ya Binza) wameishukuru TARURA kwa Bajeti hiyo kwani imegusa Mahitaji Muhimu ya Wananchi ambao wanawatumikia,
Picha za Matukio ya Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Maswa