Wilaya ya Maswa kuandikisha Watoto wa Darasa la Awali 13,000 kwa Mwaka wa Masomo 2023
15 December 2022, 4:47 pm
Imeelezwa kuwa Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu hadi kufikia mwezi Novemba , 2022 Imefanikiwa Kuandikisha Watoto wa Darasa la Awali Elfu Saba (7000) Sawa na Asilimia Hamsini na Mbili (52%) ya Makisio yote ya Watoto Elfu kumi na tatu (13000) Wanaotarajiwa kuandikishwa Darasa la Awali Mwaka 2023..
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh, Aswege Kaminyoge wakati akitoa Taarifa juu Uandikishaji wa Watoto Wilayani hapo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda alipofanyaziara ya Kutembelea na kukagua Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwa ajili ya Wanafunzi wataojiunga mwaka 2023.
Katika watoto wa Darasa la kwanza Mh Kaminyoge amesema kuwa hadi Novemba 30, 2022 walikuwa wameandikisha Watoto Zaidi ya Elfu kumi na moja (11000) Sawa na Asilimia 68% Kati ya Makadirio ya kuandikisha zaidi ya watoto Elfu Kumi na Sita (16000).
Aidha Mh Kaminyoge Amesema kuwa katika Ujenzi wa Vyumba wa Madarasa Jumla ya shule 29 kati ya 33 zimeshakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa huku vyumba 4 vikiwa katika hali ya Ukamilishaji wa Sakafu na uwekaji wa madirisha ya Alminium.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda amempongeza Mkuu wa Wilaya na Timu yake kwa zoezi la Uandikishaji wa Watoto na Kumtaka hadi kufikia Tarehe 20 mwezi huu awe amekamilisha ili mwezi Januari Wanatoto waanze Masomo bila wasiwasi.
Mh Dkt Nawanda amefanya ziara ya Ukaguzi wa vyumba vya Madarasa katika Shule ya Sekondari Nyalikungu, Shule ya sekondari Kinamwigulu, Shule ya Sekondari Buchambi Pamoja na Shule ya Sekondari Zanzui kisha kumalizia Mkutano wa Hadhara wa Kupokea Kero za Wananchi katika Uwanja wa Madeko Mjini Maswa.
Hapa chini ni picha za Matukio ya Ziara ya Mh RC Nawanda