Wananchi wa kijiji cha Zebeya Wamemshukuru Rais Samia kwa kutoa Fedha Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.6
11 October 2022, 5:03 pm
- Wananchi wa kijiji cha Zebeya kilichopo Kata ya Senani Wilayani Maswa Mkoani Simiyu Wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suruhu Hasani kwa kutoa Fedha Zaidi ya Shilingi Bilioni 1.6 kwa Ajili ya Ujenzi na Ukarabati wa Bwawa la Maji la Zebeya na Ilambambasa…
Emmanuel Sule na Elisha Jackson ni Wakazi wa kata ya Senani Wilayani Maswa Wamesema kuwa kukamilika kwa Ujenzi wa Bwawa hilo utasaidia kuwaondolea Adha ya Maji waliyokuwa wanapata Pamoja na Changamoto ya Unyweshaji maji mifugo yao..
Akitoa Maelezo kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya iliyotembelea Ujenzi huo, Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Ogoma Nyamhanga amesema kuwa ni vyema Wananchi wakawa na Uelewa na Faida za Bwawa kwa kuacha Shughuli za Kibinadamu katika njia zinazoingiza maji katika Bwawa hilo..
Amesema kuwa Shughuli za kibinadamu ndio zinafanya Bwawa lijae Matope hali inayopelekea ghaarama nyingne kwa Serikali kwa kuanza kuondoa Mchanga na Tope hivyo ni vizuri Wananchi wakaacha shughuli za kilimo kando kando ya Bwawa ili kuepusha Uharibifu huo.
Aidha Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh, Aswege Kaminyoge amesema Serikali ya Wilaya itawapa Ushirikiano watu wa Bonde la Ziwa Victoria kwa kutoa Elimu kwa Wananchi juu ya Utunzaji wa Vyanzo vya Maji huku akiwaomba Watu wa Bonde kuweka Mipaka ya Bwawa ili wananchi sehemu ambazo hazipaswi kufanya shughuli za kilimo..
Naye Mkandara anayejenga Bwawa hilo Mhandisi Edward Malale amesema kuwa kazi imeshaanza na wapo kwenye Hatua ya Ujenzi wa Tuta ambalo limekuwa likibomoka mara kwa mara huku kazi yote inategemea kukamilika Mwezi Novemba mwaka huu 2022, Ambapo Bwawa hilo litanufaisha Wakazi Zaidi ya Elfu 11 na Mifugo zaidi ya Elfu 3 kutoka kijiji cha Zebeya..