WAFUGAJI WILAYANI MASWA WAASWA KUFUGA MIFUGO KISASA ZAIDI ILI KULETA TIJA
2 September 2022, 5:44 pm
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mh Simoni Maige Amewataka Wafugaji kufuga Mifugo kwa Tija ili ilete Manufaa na kuwakwamua Kiuchumi..
Mh Maige ameyasema hayo wakati wa Uzinduzi wa Josho la kuogeshea Mifugo lililojengwa katika Kijiji cha Dodoma kilichopo kata ya Mwamashimba Wilayani Maswa na kuwataka wananchi kuondokana na Utamaduni wa kufuga Ng’ombe Wengi lakini hawana Manufaa kwao..
Amesema kuwa Wafugaji wengi wamekuwa wakiishi maisha magumu huku wakiwa na Mifugo Mingi hali ambayo mifugo hiyo imegeuka kuwa Adhabu badala ya kuwasaidia kuwakwamua kiuchumi na Kipato..
Awali akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Ujenzi wa Josho hilo Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dkt James Kawamala amesema kuwa Josho limegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 19 ambapo nguvu ya Wananchi ni Shilingi Milioni 1.7 Huku Fedha nyingine zikitoka Serikali kuu..
Aidha Dkt Kawamala amesema kuwa Josho hilo litaogesha Wanyama Zaidi ya Elfu Tano Wakimo Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo Hivyo kuweza kuokoa Vifo vya Mifugo hiyo vitokanavyo na Magonjwa ya Kupe na Wadudu wengine ambao wanachangia kwa Zaidi ya Asilimia 80.
Nao baadhi ya Wafugaji wakawa na haya ya Kusema huku wakiishukuru Serikali kwa kuwaletea huduma hiyo kwani hapo Awali walikuwa wanapata Shida kuogesha Mifugo yao huku Mwenyekiti wa Kijiji hicho akiahidi kuitunza na kuilinda Miundo hiyo kwa nguvu zote.
Haapa chini picha za matukio ya Uzinduzi wa Josho la kuogeshea mifugo.