Dc Maswa Aswege Kaminyoge- “Nitawasukuma ndani wote wanaohujumu Miundo mbimu ya Maji Nikianza na Viongozi wa Serikali ya Kijiji”..
10 August 2022, 8:24 pm
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Aswege Enock Kaminyoge amesema atawasweka ndani wote wanaohujumu Miundo mbinu ya Maji huku akianza na Viongozi wa Serikali ya kijiji…
Hayo ameyasema leo wakati akiongea katika mkutano na Watendaji wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini – RUWASA na Viongozi wa Serikali ya kijiji cha Sulu kilichopo kata ya Mbaragane wilayani hapo…
Mh Kaminyoge amesema kuwa hawezi kuvumilia kuona Miundo mbiu ya Maji iliyojengwa kwa Gharama kubwa za Serikali inaharibiwa ikiwemo kukatwa Mabomba ya kusambazia Maji huku Viongozi wa Serikali ya kijiji wapo wamekaa tu..
“Haiwezekazi nitoke Ofisini kwa ajili ya kuja kulinda miundo ya Mabomba ya Maji ili yasikatwe wakati mwenyekiti wa Kijiji na Wajumbe wako mpo..
Rais Samia ameleta Fedha nyingi kwa ajili ya Miradi ya Maji ikiwepo kijiji cha Sulu lakini mmeshindwa kuilinda na kuitunza miundo mbinu hiyo na kuruhusu watu Waibe mambo ya Maji”..
Naye Meneja wa RUWASA wilaya ya Maswa Mhandisi Lucas Madaha Amesema kuwa wamekuwa wakiingia Hasara kubwa kurudishia Bomba ambazo zimekuwa zikikatwa na wananchi…
Nao baadhi ya Wajumbe wa Serikali ya kijiji cha Sulu wamemuahidi Mkuu wa Wilaya kuwa kitendo hicho hakitajirudia maana wao watakuwa walinzi wa kwanza kwa kushirikiana na Wananchi