BUSEGA YAPIGA HATUA KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI KUTOKA VIFO 145 MWAKA 2017 HADI 41 KWAKA 2021.
25 May 2022, 6:52 pm
Idara ya Afya katika Wilaya ya Busega, mkoani Simiyu, kwa kipindi cha miaka mitano imefanikiwa kupunguza vifo vya mama na mtoto kutoka 145 mwaka 2017 hadi 41 mwaka 2021.
Hayo yamesema na Mratibu wa Huduma ya Afya ya Mama Baba na Mtoto Wilayani Busega Joseph Katitweze na Muuguzi mkuu Irene Sembo Wakati wakitoa taarifa Katika Maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani.
Wamesema kuwa , wanajivunia kupunguza vifo vya mama na mtoto kutoka 145 mwaka 2017 hadi 41 mwaka 2021, Huku akitaja malengo ni kufikia vifo sifuri ifikapo 2025.
Insert 01. Joseph Katitweze na Irene Sembo Wakieleza namna walivyopunguza vifo vya Uzazi
Aidha Mratibu huyo wa Huduma ya Afya ya Mama Baba na Mtoto ameeleza changamoto zinazowakabiri katika kutimiza majukumu yao na kuhakikisha hapatokei kifo kinachotokana na Uzazi kwani Uzazi siyo Ugonjwa..
Insert 02. Joseph Katitweze akielezea changamoto zinazowakabili
Naye Mkuu wa Wilaya ya Busega Gabriel Zakaria na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya hiyo, Bi Veronica Sayore, wameahidi kutatua baadhi ya changamoto zilizondani ya Uwezo wao ili kutengeneza mazingira rafiki kwa watumishi hao
Insert 03. Mkuu wa Wilaya ya Busega na Mkurugenzi mtendaji wakielezea namna watakavyotatua changamoto za wauguzi..
Siku ya wauguzi husherehekewa Mei 12 kila Mwaka, ikiwa kumbukumbu ya kuzaliwa muasisi kada hiyo Florence Nightngale, ambaye ni mwana takwimu na mwanzilishi wa uuguzi wa kisasa.
.
Insert 01. Joseph Katitweze na Irene Sembo Wakieleza namna walivyopunguza vifo vya Uzazi
.
Insert 02. Joseph Katitweze akielezea changamoto zinazowakabili
.
Insert 03. Mkuu wa Wilaya ya Busega na Mkurugenzi mtendaji wakielezea namna watakavyotatua changamoto za wauguzi..