Vijana Jitokezeni katika Vituo vya Huduma Rafiki ya Afya ya Uzazi.
28 March 2022, 10:19 am
Vijana wameaswa kujitokeza katika Vituo rafk vya kutolea huduma za Afya ili kupata Elimu zaidi kuhusu masuala mbalimbali ya Afya na Afya ya Uzazi.
Hayo yamesemwa na Dr Godfrey Christopher kutoka Kituo cha Afya Muungano kilichopo Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu Wakati akitoa Elimu ya afya ya uzazi kwa vijana na Umuhimu wake kupitia Sibuka fm na kusema vituo hivyo ni muhimu kwani ni sehemu sahihi ya kupata Taarifa sahihi..
Akitoa fafanuzi kuhusu huduma Rafiki za Afya ya Uzazi kwa vijana Dr Christopher amesema kuwa huduma hizo hutolewa kwa Usalama na Ufanisi wa hali ya juu hivyo vijana wajitokeze kwa wingi kupata Elimu kuhusu Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango.
Michael Luvinga ni Mratibu wa Huduma Rafiki ya Afya ya Uazi kwa vijana amesema kumekuwa na mafanikio makubwa toka kuanzishwe kwa vituo hivyo vya Huduma rafk ya Afya ya Uzazi kwa Vijana Ukilinganisha na hapo Awali .