Katibu Tawala Wilaya ya Maswa awaasa viongozi kuwatumikia Wananchi..
25 February 2022, 12:30 pm
Katibu Tawala wilaya ya Maswa Agnes Alex amewataka viongozi waliopewa Dhamana ya Kuwatumikia wananchi wanawatumikia kikamilifu ili kukidhi matarajio yao.
Katibu Tawala ameyasema hayo wakati wa Uzindunduzi wa Kikao cha Uraghbidhi kilichofanyika Februari 22, katika Ukumbi wa Halmashauri ya Maswa na Kusema kuwa wananchi wamekuwa na matarajio makubwa kutoka kwa Viongozi wao..
Bi Agenss amesema kuwa Takwimu zilizotolewa na Shirika la Twaweza zitawasaidia katika kushughulikia Changamoto zinazowakabiri wananchi wa Wilaya Maswa na siyo kuzibeza na kuzikosoa kwani zimetoka kwa Wananchi Wenyewe..
Awali akiwasilisha Taarifa ya Shughuli za Uraghbishi wilayani Maswa, Afisa Mwandamizi kutoka Shirika la Twaweza Richard Temu amesema kuwa katika Tafiti zao walibaini kuwa wananchi hawahudhurii mikutano ya vijiji kwasababu haizungumzii vipao mbele vyao badala yake viongozi kuja na Ajenda zao na siyo kusikiliza kero za Wananchi.
Steven Dwese ni Diwani wa Kata ya Ng’wigwa iliyopo wilayani Maswa amesema kuwa ni kweli wakati mwingine wamekuwa wakiitisha mikutano ya vijiji lakini wananchi hawajitokezi kwa sababu ya mgongano wa kisiasa kwenye maeneo yao.
Naye Meneja program kutoka shirika la KASODEFO Marius Isavika amesema kuwa baada ya shughuli za uraghabishi kumekuwepo na Hamasa kubwa kwa viongozi na wananchi kushiriki mikutano ya hadhara kwa ajili ya kujadili shughuli za maendeleo yao..
Hapa chini ni Picha za Matukio ya Uzinduzi wa Uraghbishi -Maswa , Simiyu