Sibuka FM

SHIRIKA LA TWAWEZA E.AFRIKA WAKISHIRIKIANA NA SHIRIKA LA KASODEFA LA WILAYANI MASWA MKOANI HAPA FEBRUARY 21 MWAKA HUU LIMEFANYA KIKAO CHA PAMOJA NA WARAGHBISHI TOKA KATA 18.

25 February 2022, 12:08 pm

Shirika la Twaweza wakishirikiana na shirika la Kasodefo la Wilayani Maswa Mkoani Simiyu February 21 mwaka huu wamefanya kikao cha pamoja na waraghbishi toka kata 18.

Huku kikao hicho kikilenga kufanyia tathmini ya awali ya shughuli za kiraghbishi zinazotekelezwa katika kata 18 tu, kati ya kata 36 zilizopo Wilayani hapa.

Akizungumza na Radio Sibuka fm afisa mwandamizi idara ya ushiriki toka Twaweza amesema kuwa program hiyo inasaidia kuongeza ushiriki wa wananchi kwenye miradi ya maendeleo kama anavyobainisha.

Sauti ya Richard Temu Twaweza

Baadhi  ya uraghbishi  wiayani  hapa  wamesema kuwa program hiyo ya uraghbishi imeondoa  uwoga kwa wananchi na kuchochea utayari wa kujitolea huku kero ya Barabara ikionekana kuwa ni changamoto kijijini hapo.

Insert………Baadhi ya  Mraghbishi.

Sauti za Baadhi ya Waraghbishi

Aidha kwa upande wake meneja program toka shirika lisilokuwa la kiserikali la Kasodefo Bw,Marius Isavika amesema kuwa program hiyo imewakutanisha jumla ya  washiriki 36 huku huku program hiyo ikitekelezwa Wilayani Maswa pekeyake kwa kati ya Wilaya zote Mkoani hapa,kama anavyofafanyua.

Sauti ya Marius Isavika –Meneja Kasodefa
Washiriki wa mafunzo ya Uraghabishi wakiwa katika Mafunzo-Ndemax Maswa