KILELE CHA WIKI YA SHERIA , MAHAKAMA YA WILAYA MASWA YAPOKEA MALALAMIKO 345 , UTELEKEZWAJI WA WATOTO WAONGOZA..
8 February 2022, 9:44 am
Mahakama ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu imepokea jumla ya malalamiko 345 katika wiki ya sheria huku malalamiko ya utelekezwaji wa watoto yakiongoza yakifuatiwa na Migogoro ya Ardhi.
Akitoa taarifa kwa mgeni rasimi, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Maswa Christiani Lugumira amesema kuwa katika utekelezaji wa wiki ya sheria mahakama ilikuwa na jukumu la kuwaeleza wananchi maboresho ambayo yamefanyika kwa Faida ya wananchi
Katibu Tawala wa Wilaya ya Maswa Agness Alex kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya Aswege Kaminyoge amesema kuwa Wananchi bado wanahitaji kuelimishwa juu ya masuala ya kisheria kwani wanahitaji Huduma ya Mahakama kwa Ukaribu Zaidi.
Naye mwakilishi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika – TLS Janeth Masige amesema kuwa sehemu pekee ambayo mwananchi anaweza kupata Haki yake ni Mahakama ambapo TLS ni wadau hivyo wananchi wazitumie Mahakama katika utoaji haki.
Marselina Francis ni Afisa wa Jeshi la Polis Dawati la Jinsia na Watoto wilayani Maswa Amesema kuwa kumekuwepo na kesi nyingi za utelekezwa wa watoto kutokana na Baadhi wa wazazi kuzikimbia Familia zao hali inayopelekea ongezeko la Watoto wa Mitaani
Baadhi ya Watoto walioshiriki kilele cha wiki ya Sheria wilayani Maswa wamesema kuwa Serikali itunge sheria Kali na kuzisimamia kwa wazazi wanaotelekeza watoto wao.
Maadhimisho haya ya wiki ya Sheria kwa Mwaka huu 2022 yamebeba Kauli mbiu ya DHAMA ZA MAPINDUZI YA NNE YA VIWANDA, SAFARI YA MABORESHO KUELEKEA MAHAKAMA MTANDAO.