kata saba wilayani bariadi kuunganishwa na miundombinu ya barabara
30 January 2022, 2:59 pm
Na mwandishi wetu Daniel Manyanga,Simiyu
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi wameshauri kuunganishwa kwa kata saba kwa njia ya barabara ili kuwapunguzia adha wananchi kutumia muda mrefu kufika makao makuu halmashauri hiyo yaliyopo Dutwa.
Wameyasema hayo wakati wakipokea taarifa kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo cha kupitia rasimu ya bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/23 kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Dutwa.
Awali akitoa taarifa kaimu meneja wa wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA wilaya ya Bariadi mhandisi Nyamagalula Ndango amesema wanajumla ya km 607.49 huku akiongeza kuwa halmashauri hiyo iliidhinishiwa kiasi cha shilingi bilioni 2.4 kwaajili ya matengenezo ya barabara,makaravati katika utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022.
Amesema TARURA Bariadi inatekeleza miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2 kwa mwaka wa fedha 2021/22 na hadi sasa utekelezaji umefikia asilimia 40 huku bajeti ya matengenezo ya barabara ,madaraja na makaravati kwa mwaka wa fedha 2022/23 ukikadiriwa kutumia shilingi bilioni 2.4
kaimu meneja TARURA wilaya ya Bariadi mhandisi Nyamagalula Ndango
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange amewaomba madiwani kuwa sehemu ya usimamizi wa barabara huku katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Bariadi Masanja Sallu akishauri wakandarasi kutopewa kazi nyingi
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange