Sibuka FM

WAWILI WAPOTEZA MAISHA ,WANNE WAJERUHIWA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI MGODINI

6 January 2022, 11:19 am

Na mwandishi wetu Daniel Manyanga,Simiyu

Watu wawili wamepoteza maisha huku wengine wanne wakijeruhiwa baada ya kufunikwa na kifusi kwenye mgodi wa dhahabu wa Halawa no 2 uliopo halmashauri ya wilaya ya Bariadi .

Akithibitisha kupokea miili na majeruhi wa tukio hilo kaimu mganga mfawidhi wa kituo cha afya Byuna Dkt Deogratius Mtaki amesema mara baada ya kupokea taarifa walifika kwenye eneo la tukio na kukuta tayari watu wawili wamepoteza maisha.

Aidha Dkt Mtaki aliwataja majeruhi kuwa ni John Deus Tibasila ( 36) mkazi wa Msalala ambaye alikuwa ameumia kwenye paji la uso, Joseph Sendama Masalu (28) mkazi wa Kahama alivunjika mkono ,Mahanga Marwa (45)mkazi wa Serengeti na Wambura Kichere Maswi (29)mkazi wa Rorya wao walipata majeraha sehemu mbalimbali na walipatiwa matibabu ya awali kabla ya kupewa rufaa kwenda hospitali ya rufaa ya Bugando iliyopo jijini Mwanza .

Mbali na majeruhi hao Dkt Mtaki aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni Hamis Emmanuel (32)mkazi wa Masumbwe na Yusuph Manyangi (32).Insert ya Dkt Mtaki

Sauti ya kaimu mganga mfawidhi kituo cha afya Byuna Dkt.Mtaki akithibitisha kupokea miili ya majeruhi na marehemu wa tukio la mgodini

Awali katibu  msaidizi  idara ya ukaguzi mgodi wa Halawa no 2 Laurent Misango  amesema tukio lilitokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia Jan 4,2022  ambapo baada ya kutokea kwa tukio hilo idara ya ukaguzi kwa kushirikiana na idara ya ulinzi wakiwemo askari polisi walifika eneo la tukio duara no 94 B  ambapo idara ya ukaguzi iliingia ndani kujiridhisha kuhusu taarifa hiyo.

Sauti ya katibu msaidizi wa idara yaukaguzi mgodi wa Halawa no 2 Laurent Misango

Sitta Bugali  ni mmoja wa wachambaji na pia ni miongoni  mwa watu walioingia ndani ya duara hilo (94 B) kuokoa amesema alibahatika kuokoa majeruhi wawili na kuitoa miili  miwili huku akieleza kuwa walipofika chini walikuta udongo wa kwenye  duara umeporomoka na kuwakandamiza waliokuwa ndani ya duara hilo.

Sauti ya mmoja wa mashuhuda wa tukio la mgodini ndugu Sitta Bugali