Mkoa wa Simiyu wapunguza vifo vitokanavyo na Uzazi kwa Asilimia 50% Mwezi Julai – Septemba, 2021
27 November 2021, 6:28 pm
Mkoa wa Simiyu umefanikiwa Kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi kwa Asilimia 50% kwa Robo ya mwezi Julai, August na mwezi Septemba 2021 huku Upatikanaji wa Dawa Ukiongezeka kutoka Asilimia 70% hadi kufikia Asilimia 90%.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mheshimiwa David Zacharia Kafulila katika kikao kazi cha Wadau wa Afya kilichofanyika Mjini Bariadi na Kusema kuwa kupungua kwa vifo hivyo ni kutokana na Usimamizi mzuri wa Sekta ya Afya kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali wa Afya
Mheshimiwa Kafulia amesema kuwa mkoa wa simiyu umejipanga kwa kila mtendaji wa sekta ya Afya atapimwa kwa alama katika Utoaji wa Huduma kuanzia Ngazi ya Zahanati hadi Mkoa
Kwa upande wake Mganga mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dr Boniphace Malwa amesema kuwa pamoja na kufanikiwaa kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi kwa Asiimia 50% bado vituo vingi vya afya havijafikia Malengo ya kutoa huduma bora kwa Jamii hali inayopelekea malalamiko mengi kwa Wananchi..
Insert 03. Dr BONIPHACE MALWA
Aidha Mratibu wa Chanjo ya UVIKO -19 Mkoa wa Simiyu akatoa Taarifa kuhusu mwenendo wa zoezi na Idadi ya watu waliochanjwa hadi kufikia mwezi wa 10, 2021.