zaidi ya bilion 10.8 kutatua changamoto ya maji hasa vijijini mkoani simiyu
30 October 2021, 7:59 am
Na mwandishi wetu Daniel Manyanga,Simiyu
Zaidi ya bilioni 10.8 zilizotolewa na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Samia Suluhu Hassan zikiwemo zaidi ya bilioni 8 za bajeti ya kawaida na zaidi ya bilioni 2 ambazo ni fedha za uviko -19 mkoani Simiyu zinaenda kuondoa adha ya maji vijijini.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila akiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Itilima iliyopo mkoani hapo na kumpongeza rais wa awamu ya sita Mhe,Samia Saluhu Hassan kwa kuzitumia fedha za uviko-19 kutekeleza miradi ya maji ambapo zingeenda kununua vifaa vya kukabiliana na ugonjwa wa corona .
Mbali na hilo amesema kuna mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa victoria ambapo maji yatafikishwa mkoa hapo kupitia bomba lenye urefu wa km 194 wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 400 ambapo vijiji 244 vitanufaika mkoani hapo na kwenda kupunguza adha ya ukosefu wa maji hasa vijijini.
Kafulila amesema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili upatikanaji wa maji ulikuwa asilimia 40.5 na sasa umefikia asilimia 67.5 sawa na ongezeko la asilimia 27 ambapo ameongeza kuwa maji ni bidhaa na huduma muhimu pengine kuliko zote.