walimu wilaya ya itilima waomba kutatuliwa changamoto zao.
27 October 2021, 2:51 pm
Na mwandishi wetu Daniel Manyanga ,Simiyu
Walimu wilayani Itilima mkoani Simiyu wameiomba serikali kuona umuhimu wa kutatua changamoto zao ili kuongeza hali ya utedaji kazi.
Wameyasema hayo kwenye semina ya kuwajengea uwezo kwenye majukumu yao viongozi na wawakilishi wa shule wa kutoka Chama Cha Walimu (CWT) wilaya ya Itilima.
Awali akisoma risala mbele ya mkuu wa wilaya hiyo ambaye alikuwa mgeni rasmi katibu wa chama Cha walimu (CWT) wilaya ya Itilima Njile Lufasinza amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili walimu huku mhasibu wa chama hicho Masuka Ikongo amesema swala la kupandishwa madaraja kwa walimu waliokidhi vigezo lipewe kipaumbele na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Akijibu namna ya kutatua changamoto hizo mkuu wa wilaya ya Itilima Faiza Salim amesema tayari serikali ameanza jitihada za utatuzi wa baadhi ya changamoto zinazowakabili walimu.
Katika hatua nyingine katibu tawala wa wilaya hiyo Firbert Kanyilizu amewataka walimu wenye tabia ya kukopa bila malengo kuacha mara moja kwani tabia hiyo siyo nzuri.