Sibuka FM

hakielimu yatoa mafunzo na vyerehani kwa watoto wa kike ili kushona taulo za kike

13 October 2021, 2:30 pm

Katika kukabiliana na changamoto za watoto wa kike kutohudhuria kikamilifu masomo yao hakielimu kupitia mradi wa  The Girls Retention and Transition Initiative (G.R.T.I ) imetoa vyerehani na mafunzo kwa wanafunzi kutegeneza taulo za kike ili waweze kujihifadhi kipindi cha hedhi .

Hayo yamesemwa na walezi wa vinara kupitia mradi wa G.R.T. I  ambapo wameongeza kuwa kabla ya mafunzo hayo baadhi ya watoto wa kike hususan wanafunzi walikuwa wanatumia vitu ambavyo ni hatari kwa afya zao.

Sauti ya walezi wa vinara kupitia mradi wa G.R.T.I

Janeth Jackson ni afisa ustawi wa jamii kutoka halmashauri ya mji wa Bariadi amesema  kuwa vitendo vya ukatili vinatolewa taarifa zikiwa zimecheleweshwa huku afisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya mji wa Bariadi  Hollo Ngeme akiongea kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo amewapongeza  haki elimu  kwa kutoa mafunzo ya namna ya kutengeneza taulo za kike.

Sauti ya afisa ustawi wa jamii halmashauri ya mji wa Bariadi Janeth Jackson pamoja Hollo Ngemeafisa maendeleo ya jamii halmashauri ya mji wa Bariadi

Nao baadhi ya wanafunzi wameomba jamii hususan wazazi na walezi wawe wanapewa elimu dhidi ya kupinga vitendo vya  ukatilii wa kijinsia huku wakiwaomba watoto wa kike wasirubuniwe ili na wao wafikie malengo yao.

Sauti ya wanafunzi walifanikiwa kupata mafunzo na vyerehani ili kuweza kushona taulo za kike


Maadhimisho hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza mkoani hapa yakiwa na kauli mbiu isemayo “kizazi cha kidijitali ,kizazi chetu” huku yakienda sambamba na maigizo na burudani kutoka kwa wanafunzi wa vinara kutoka  baadhi ya shule za msingi na sekondari zilizopo mkoani hapa.