NMB yatoa Msaada wa vifaa vya ujenzi Shule za Msingi na Sekondari Maswa.
8 October 2021, 7:15 pm
Benki ya NMB imekabidhi vifaa vya Ujenzi kwa Shule za Msingi na Sekondari Wilayani Maswa Mkoani Simiyu vyenye thamani ya Shilingi Milioni Ishirini na Nne..
Akikabidhi vifaa hivyo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge , Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Magharibi Ndugu Sospeter Magesse amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kukamilisha Ujenzi wa vyumba vya Madarasa na kupunguza adha ya Michango kwa Wananchi..
Bwana Magesse amezitaja shule zilizopata misaada hiyo na kusema kuwa Benki ya NMB imekuwa na utaratibu wa kila mwaka kurudisha asilimia ya faida yake kwa Wananchi na kuzielekeza katika sekta ya Elimu na Afya.
Akipokea vifaa hivyo kwa Niaba ya wananchi Mkuu wa wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge amesema kuwa anawashukuru Benki ya NMB na kuahidi kuvitunza na kutumika kama ilivyoelekezwa huku akimwelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kutatua changamoto za miundo mbinu ya Barabara , Umeme na maji katika shule hiyo ya Msingi Mwawai ..
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mh Paul Maige amesema kuwa NMB imeonyesha mfano kwa kuunga mkono jitihada za Serikali za ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuleta maendeleo kwa wananchi..
Wakitoa shukurani zao kwa Benki baadhi ya wanafunzi wa shule ya Mshingi Mwawai wamesema kuwa vifaa hivyo vitawasaidia kukaa kwenye madarasa bila kubanana na kuwafanya wasome vizuri huku wakielekeza kilio chao kwa serikali kuwaboresha miundombinu ya Barabara kwani kipindi cha Masika kumekuwa hakufikiki shuleni hapo…
Hapa chini ni picha za matukio ya kukabidhi vifaa vya Ujenzi- shule ya Msingi Mwawai