Sibuka FM

Mhe, BEREGE akabidhiwa Ofisi aahidi neema kwa wana Maswa

13 August 2021, 10:12 am

Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Halmashauri  ya  wilaya  ya  Maswa   Mkoani  Simiyu   Ndugu  Saimoni  Berege  ameahidi  kutoa  ushirikiano  kwa  Madiwani  na  watumishi   wa kada  mbalimbali  pamoja  na   kwakuendeleza  miradi  yote  ambayo  ilianzishwa  na  Mtangulizi  wake  Dr  Fredrick   Sagamiko   ambaye  kwa  sasa  amehamishiwa  Manisipaa  ya  Songea   Mkoani  Ruvuma.

Hayo  ameyasema   wakati  wa  Makabidhiano  ya  Ofisi  kati  ya  Mkurugenzi  huyo  mpya  na  Mkurugenzi  ambaye   aliyehamishiwa    Manispaa  ya  Songea   na    kusema  kuwa   maendeleo    yanaletwa   kwa  Ushirikiano  wa  Serikali  na   Wananchi..

       

Saimon Berege
Sauti ya DED mpya Maswa Saimoni Berege

Amesema  kuwa   yeye   ataongoza  kwa  kufuata  Sheria,  kanuni  na  taratibu za  Kiserikali  hivyo  Watumishi  waache  kufanya  kazi  kwa  mazoea  kwani  yanazorotesha  maendeleo  ya  wananchi.

        

Sauti ya DED mpya Maswa Saimoni Berege

Naye  mwenyekiti  wa   Halmashuri  ya  Wilaya  ya  Maswa  Mh,  Paul   Simoni  Maige  amesema   kuwa  mambo  mengi  amejifunza  kutoka  kwa  aliyekuwa  Mkurugenzi    Dr  Sagamiko  ambayo  yanamsaidia  katika kuongoza   Halmashauri.

Sauti ya Mwekiti wa Halmashauri- Paul Maige

        

Aidha  akikabidhi  ofisi  aliyekuwa  mkurugenzi  wa  Halmashauri  ya  hiyo  Dr   Fredrick  Sagamiko   amewashukuru   Watumishi  na  wananchi  wa  wilaya  ya   Maswa  kwa  Ushirikiano  waliompatia  katika kutekeleza  majukumu  yake    hivyo  amekabidhi  halmashauri  kwa  Mh   Berege  katika  mikono  Salama    wananchi  wasiwe  na   wasiwasi..

Sauti ya DED aliyeondoka Fredrick Sagamiko

         

Hapa chini ni Picha mbalimbali za makabidhiano na maeneo waliyotembelea.

Mkono wa kulia aliyevaa shati nyeupe kwa ndani ni Dr Fredrick Sagamiko aliyehamia Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma,, Mwenye Suti ya Dark blue ni Mh Saimoni Berege Mkurugenzi mtendaji mpya halmashauri ya wilaya ya Maswa