Maji ya Ziwa Victoria kuleta suruhisho la changamoto ya maji mji wa malampaka-Simiyu.
22 July 2021, 10:47 am
Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya maji na Usafi wa mazingira Maswa- MAUWASA Mhandisi Nandi Mathias amesema kuwa kuanza kutekelezwa kwa mradi wa maji kutoka ziwa Victoria utaondoa changamoto ya Upatikanaji wa Maji katika katika Mji wa Malampaka uliopo wilayani Maswa Mkoani Simiyu.
Mhandisi Nandi amesema kuwa mji wa malampaka unawakazi zaidi ya Elfu kumi na tano ikiwa mahitaji ya maji kwa siku ni Lita za Ujazo milioni moja hali inayopelekea kuwa na Upungufu ikilinganishwa na Uzalishaji wa maji kwa siku..
Amesema kuwa changamoto zilizojitokeza wakati wa Mkutano wa hadhara wa mkuu wa mkoa kwa baadhi ya wananchi kusema visima havitoi maji siyo kweli kwani visima hivyo kwa sasa vinafanya kazi na walivifufua baada ya kukabidhiwa kutoka kwa Wakala wa Usambazaji maji na Usafi wa Mazingira vijijini –RUWASA.
Yona Gabriel Swale na Angela Masunga ni wasimamizi katika pampu za kusukuma maji katika mji wa malampka wamesema kuwa changamoto ya maji ipo ikilinganishwa na wingi wa Watu licha ya wao kusukuma maji kwa wakati..
Aidha baadhi ya wananchi wamezungumza Radio Sibuka na kusema kuwa hali ya upatikanaji wa maji kwa sasa katika mji huo ni nzuri ikilinganishwa na hapo awali maji yalikuwa ya shida upatikanaji wake.
Hapa chini picha mbalimbali..