Mradi wa Chujui la Maji Maswa wanufaisha wakazi zaidi ya Laki moja.
23 June 2021, 10:15 am
Zaidi ya wakazi Laki moja wa Mji wa Maswa na vijiji jirani wamenufaika na Mradi wa Mtambo wa kutibu na Kusafisha Maji.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Maswa-MAUWASA Mhandisi Nandi Mathias wakati wa kutembelea Ujenzi wa Mradi huo uliogharimu Zaidi ya Bilioni tatu.
Mhandisi Nandi amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo maji umeondoa adha ya upatikanaji wa maji kwani kwa sasa Unazalisha lita za Ujazo Elfu kumi ikiwa Mahitaji maji kwa Mji wa Maswa ni lita za Ujazo elfu Saba.
Bahati Mwaipopo ni Mhandisi kutoka kampuni ya PET CO-OPARATION LIMITED ambao ndio wajenzi wa Mradi huo amesema kuwa kwa sasa Mradi huo umekamilika kwa asilimia mia moja.
Aida baadhi ya wananchi na wadau wa maji mjini maswa wameishukuru serikali kwa kujenga chujio hilo kwani kwa sasa maji yanatoka meupe na ang’avu tofauti na hapo awali kabla ya kukamili kwa mradi wa ujenzi wa Chujio hilo..
Picha za muonekano wa Mradi wa Chujio na Chanzo chake- Bwawa la New Sola.