chama cha mapinduzi (ccm) mkoa wa simiyu chapata mwenyekiti mpya
23 May 2021, 8:07 am
Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Simiyu leo kimefanya uchaguzi wa kumpata mwenyekiti wa chama hicho ili kuziba nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Enock Yakobo aliyefariki februari 23 ,2021.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo msimamizi wa uchaguzi huo Wilbroad Mutabuzi amesema kura zilizopigwa ni 704 na hakuna kura iliyoharibika ambapo amemtaja Shemsha Mohamed kuibuka kidedea kwa kura 441 akifatiwa na Alphonce Kinamhala kwa kura 174 huku Sakina Omari akishika nafasi ya tatu kwa kura 89.
Akitoa neno la shukrani mwenyekiti huyo ameahidi kufanya kazi kwa ushirikiano na kila mmoja huku akiongeza kuwa uchaguzi umekwisha kilichobaki ni kuisimamia ilani ya chama hicho.
Awali akiongea kwa niaba ya wabunge wa mkoa huo ,mbunge wa Itilima Njalu Silanga amewaomba wanasimiyu hususan kuhakikisha mkoa unazidi kusonga mbele kimaendeleo huku akiongeza kuwa wao ( wabunge) wapo mstari wa mbele katika kiwatumikia wananchi.
Nae katibu mwenezi wa chama hicho mkoa wa Simiyu Mayunga George amewapongeza wajumbe kwa kufanya uchaguzi kwa utulivu na kufuata taratibu za chama hicho hatua iliyopelekea kumaliza kwa amani.
“Niwapongeze sana wanachama wote ambao mumeshiriki kikamilifu katika zoezi zima la kumpata mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa mmeonesha ukomavu wa kisiasa kwa kufanya uchaguzi kwa amani hadi tumemaliza na huo ndio msingi wa chama cha mapinduzi asanteni sana “amesema Mayunga George