Zaidi ya Ng’ombe laki tatu kuchanjwa wilayani Maswa
20 April 2021, 10:28 am
Zaidi ya Ng’ombe laki tatu wilayani Maswa mkoani Simiyu zinatarajiwa kuchanjwa ili kudhibiti Magonjwa ya Mifugo ikiwemo Ugonjwa wa Mapele ya ngozi ili kuboresha bidhaa ya ngozi na Ushindani wa Soko..
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge, Daktari wa Mifugo wa wilaya Dokta James Kawamala amesema kuwa endapo wafugaji watashindwa kuchanja wataendelea kuhatarisha Maisha ya wanyama hao.
Sister Rozamisti Kasambu ni Daktari wa Mifugo na Afisa Mfawidhi Kanda ya Ziwa amesema kuwa mfugaji yoyote ni lazima awapende mifugo wake kwa kuwapeleka kwenye Chanjo zinazotolewa na wataalamu wa mifugo.
Akizindua zoezi hilo la chanjo ya Mifugo Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Kminyoge amesema kuwa kila mfugaji ahakikishe anapeleka Mifugo yake yote kwenda kuchanjwa bila kuacha baadhi ya mifugo Nyumbani ..
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Paul Simon Maige na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Paul Jidayi wamesema kuwa Zoezi ni la Muhimu hivyo ni vyema kufuata maelekezo ya Wataalamu.
Aidha kwa upande wa wafugaji wameishukuru Serikali kwa kusimamia zoezi hilo la Chanjo kwani litasaidia Kuboresha mifugo yao..