Sibuka FM

WANNE WAFA MGODINI,MMOJA AKIJERUHIWA

14 April 2021, 5:08 pm

Wachimbaji wadogo  wanne wa dhahabu wafariki dunia na mwingine kujeruhiwa baada ya kuporomoka kwa kuta wakati wakiendelea na uchimbaji wa dhahabu kwenye duara zao katika mgodi wa dhahabu na 2 uliopo Imalamate wilayani Busega mkoani Simiyu.

Kwenye picha ni RPC mkoa wa Simiyu ACP Abwa0

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu ,kamishina msaidizi wa polisi,Richard Abwao amesema kuwa tukio hilo limetokea  mnamo majira ya saa 22:25 usiku wa tarehe 12.04.2021 huko katika Kijiji na kata ya Imalamate tarafa ya kivukoni wilayani Busega.

ACP  Abwao, amewataja  waliofariki dunia katika tukio hilo kuwa ni  Limbu Kisabo miaka 28 msukuma mkazi  wa Kijiji cha Mwakibuga-Bariadi,Tembo Male miaka 42 msukuma mkazi wa wa Kijiji cha Isanga,Benjamini Masaka miaka 51 msukuma mkazi wa  Katoro-Geita na Musa Washa miaka 37 msukuma mkazi wa Kijiji cha Isengwa-Bariadi huku aliyejeruhiwa ni Mangu Ngumba miaka 33 msukuma wa Bariadi na miili ya marehemu imepelekwa hospitali ya Somanda kwa ajili ya uchunguzi.

Ambapo katika tukio hilo lililotokea wakati  wachimbaji wadogo hao wakiendelea na shughuli ya uchimbaji dhahabu  katika duara no 18 AB na 17 AB eneo la Trencha ambapo kuta ziliporomoka na kusababisha vifo hivyo Pamoja na majeruhi huku chanzo kikitajwa kuwa ni mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapo.

Insert ya Rpc Simiyu 1

Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani hapo limetoa wito kwa wachimbaji wadogo wote kuchukua tahadhari za kiusalama katika shughuli zao hasa katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha mkoani hapo.

Insert ya Rpc Simiyu 2