Chai FM

Kamati ya Bunge ya uongozi ya serikali za mitaa [TAMISEMI ] yaridhishwa ujenzi wa barabara Rungwe

16 March 2022, 10:41 am

RUNGWE

Na Lennox Mwamakula

Kamati ya Bunge ya uongozi ya serikali za mitaa [TAMISEMI ] imefanya ziara wilayani Rungwe mkoani  Mbeya  ya ukaguzi wa barabara  ya kutoka   Masebe-Bugoba hadi Lutete yenye urefu wa kilometa 12 iliyo jengwa kwa kiwango cha lami na kuridhishwa na ujenzi huo. 

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa barabara hiyo mhandisi wa tarura mkoa wa Mbeya  Wilson Charles amesema uwepo wa barabara hiyo kumewarahisishia wananchi  waishio maeneo hayo kusafirisha mazao yao kwa urahisi  kwani kumekuwa na ongezeko kubwa la uzalishaji wa mazao ya biashara.

Akipokea taarifa hiyo mwenyekiti wa kamati hiyo Mh. Abdallar Chaulio ameupongeza uongozi wa mkoa wa mbeya kwa ushirikiaano mzuri wanao uonyesha  katika utekelezaji wa miradi  mbalimbali  na amewaomba mameneja wa TARUA wa wilayani kuwashirikisha wabunge  ili kuweza kusaidiana pale panakuwa na changamoto

Waziri Innocent Bashungwa wa kwanza kulia akitoa maelekezo kwa kamati ya Bunge ya uongozi ya serikali za mitaa

Kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na Serikali za mitaa [TAMISEMI] Mh, Innocent Bashungwa  ameishukuru  kamati hiyo  kwa kuridhishwa na ujenzi wa barabara hiyo na kuiomba  kamati hiyo kuona namna ya kuwepo kwa ushirikiano  baina ya TANROADS na TARURA  ili kuweza kukamilisha  kipande cha barabara cha  kutoka  ushirika  Mjini hadi  Masebe chenye urefu wa kilometa moja ambacho kipo chini ya TANROADS

Naye mkuu wa mkoa wa mbeya mh, Juma Homera  amesema kuwa barabara zote zinazo jengwa ofisi ya mkuu wa mkoa imetoa maagizo kufungwa taa za barabarani ili wanachi waweze kutumia  barabara hizo kwa yakati zote

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya bunge ya uongozi ya serkali za mitaa wakiongozana na baadhi ya watumishi wa wilaya ya Rungwe katika ukaguzi wa barabara ya masebe- bugoba hadi Lutete