

18 March 2025, 9:20 pm
“Elimu ya usalama barabarani bado haikwepeki hivyo mamlaka husika zinao wajibu wa kutoa elimu hasa kwa makundi ambayo yanaweza kuwa msaada mkubwa wa kufikisha elimu kwa jamii kubwa”.
Na, Daniel Manyanga
Katika kuhakikisha ajali za barabarani zinaisha au kupungua mkoani Simiyu Wanafunzi wametajwa kuwa mabalozi wazuri wa utoaji wa taarifa za usalama barabarani kwenye jamii inayowazunguka hali inayotajwa kuwa njia bora ya kuifikia idadi kubwa ya wananchi Ili kumaliza ajali hizo.
Wakizungumza na Sibuka fm wakati wa utoaji elimu hiyo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Sima B mjini Bariadi,Manjale Magembe ambaye ni mwenyekiti wa RSA mkoa na Alchangela Kashemeza katibu wa RSA mkoa huo wamesema lengo la utoaji elimu ya usalama barabarani katika kundi hilo ni kutanua wigo wa elimu kwa jamii ili kuweza kumaliza changamoto za ajali barabarani.
CPL,Lutego Buswelu ni askari wa usalama barabarani wilayani Bariadi amesema kuna kila sababu ya kila mtumiaji wa barabara kizingatia sheria za usalama wa barabarani katika kumaliza ajali ambazo siyo za lazima
Wakiongea kwa niaba ya wanafunzi ,Isaka Mauna na Felister Daniel wamesema kuwa ujio wa elimu hiyo utasaidia kupunguza ajali za barabarani kwa kuwa wamejuwa baadhi ya alama muhimu za usalama barabarani.