

12 March 2025, 6:07 pm
“Hoja za madereva wa daladala mkoa wa Simiyu naomba zisikilizwe maana kuna hoja kubwa sana ni kweli serikali yangu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania imejenga stund tena nzuri kweli ya kisasa lakini sasa hatuwezi kuwachanganya hawa tunaenda kuua biashara yao naomba busara zitumike katika kushughulikia hili maana Kambare ni mkubwa hivyo chakula chake ni dagaa wadogo”.
Na, Daniel Manyanga
Madereva wanaoendesha magari madogo ya abiria mkoani Simiyu wamegoma kwa siku mbili mfululizo kufanya safari lengo likiwa kuishinikiza serikali kuwatengea eneo la kupakia abiria tofauti na sasa ambapo wanatakiwa kupakia stand kuu ya mabasi hali ambayo imetajwa kuwanyima riziki mkoani hapo.
Akizungumza na Sibuka fm makamu mwenyekiti wa umoja wa daladala mkoa wa Simiyu,Mussa Pomokela amesema kupakia stund kuu ya mabasi ya mkoa ni kuwanyima riziki za wao kupata abiria kutokana kuwepo kwa mabasi mengi makubwa yanayofanya safari kuanzia hapo hapo stund hivyo ngumu kwa abiria kupanda gari ndogo.
Akijibu malalamiko hayo mkuu wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga amesema ni vema madereva hao wakafuata sheria zilizopo na siyo serikali ya wilaya ifate kile wao wanachokitaka maana tayari serikali ya imeshajenga stund ya mabasi ya mkoa na kuna eneo la kupakia kwa magari hayo madogo.
Simon Simalenga kuhusu baadhi ya magari kukamatwa ametoa maagizo kwa mamlaka zilizohusika kukamata magari hayo kuyaachia mara Moja magari yaweze kurudi kwa wenye nayo.