

26 February 2025, 11:46 am
DC mpya Wilayani Maswa Mkoani Simiyu awataka watumishi na watendaji kutafsiri maono ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwa vitendo,hali itakayoisaidia Wilaya hiyo kupiga hatua za kimaendeleo.
Na,Paul Yohana-Maswa-Simiyu
Mkuu mpya wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Dkt,Vincent Anney amewaomba watumishi wa taasisi mbalimbali na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama Wilayani hapa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kufikisha maendeleo kwa wananchi.
hayo yamesemwa na Dkt,Anney mara baada ya kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh,Aswege Kaminyoge.
Aidha Dkt.Anney amehimiza kufanya kazi kama timu na mtumishi yeyote akiona jambo lolote ambalo linahusu wilaya ya Maswa asisite kutoa taarifa mapema ili kufikia ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hasan ya kufikisha maendelo kwa jamii
Kwa upande wake aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Maswa Mh.Aswege Kaminyoge ambae kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mkoani Mara akitoa taarifa kwa mkuu mpya wa Wilaya ya Maswa Dkt, Anney amesema kuwa Wilaya ya Maswa imetekeleza miradi mingi ndani ya kipindi cha miaka (4)ya utawala wa Dkt,Samia.