

26 February 2025, 10:34 am
Watumishi wilayani Maswa mkoani Simiyu wakumbushwa kuwajibika kwa weledi ili kuendana na kasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Na,Alex Sayi-Maswa Simiyu
Mkuu mpya wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Dkt, Vincent Anney amewakumbusha watumishi Wilayani hapa kuhakikisha wanawajibika kikamilifu ili kuwasogezea maendeleo wananchi.
hayo yamesemwa na Dkt,Anney mara baada yakukabidhiwa ofisi hiyo na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Mh,Aswege Kaminyoge aliyehamishiwa kituo Kipya cha kazi Wilaya ya Bunda Mkoani Mara,kufuatia mabadiriko madogo yaliyofanywa na Rais Samia Februari,21/2025
Awali Dkt,Anney akizungumza kwenye makabidhiano hayo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt,Samia Suluhu Hasani kwakuendelea kumwamini kwenye majukumu hayo ya ukuu wa Wilaya,huku akibainisha kuwa kwenye utumishi wake siyo muumini wa utendaji kazi wa michakato
Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge amemshukuru Rais Samia kwakumwamini kuendelea na majukumu yake ya ukuu wa Wilaya
Aidha kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Maswa Athuman Kalaghe akishukuru kwa niaba ya watumishi wa ofisi hiyo alimtakia kilalakheri aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Mh,Aswege Kaminyoge(a.k.a,Professor )