

25 February 2025, 6:17 pm
Kiwanda cha kuzalisha chaki kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu mbioni kuzalisha chaki zitakazokuwa mwarobaini kwa mahitaji ya chaki nchini kwa shule za msingi na sekondari.
Na,
Alex Sayi
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu iko mbioni kuanza uzalishaji wa chaki zitakazouzwa Nchi nzima kwa shule za msingi na sekondari na nje ya Nchi.
Hayo yamebainishwa mbele ya Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara akiwa ziarani mkoani Simiyu alipotembelea kiwanda cha kuzalisha chaki kilichopo wilayani Maswa mkoani hapa Februari 23 mwaka huu.
Akisoma taarifa ya kiwanda hicho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Maswa, Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Bw. Julius Ikongora amesema kuwa kiwanda hicho kimegharimu zaidi ya Sh.Bil.10
Akizungumza na Radio Sibuka FM Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw. Maisha Mtipa amesema kuwa anaishukuru serikali ya Mama Samia kwa kutenga fedha hizo na kubainisha kuwa kiwanda hicho kitaisaidia halmashauri hiyo kuongeza mapato yake ya ndani na kupunguza utegemezi wa mapato toka Serikali Kuu
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mh,Exaud Kigahe ameipongeza Halmashauri hiyo kwa uamuzi wake wa kujiendesha kibiashara kupitia kampuni tanzu ya Ng’hami Industrial Kampani