

24 February 2025, 3:51 pm
‘‘Hakuna mtu yeyote atakayetoka nje ya nchi kuja hapa nchini kwetu kutuambia namna bora ya kulifanya taifa letu liweze kusonga mbele katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ili kufikia malengo mama ya taifa kama sisi wenyewe hatutaweza kulipa kodi kwa hiari ambapo kodi hizo ndizo zinapeleka maendeleo kwa wananchi tulipeni kodi kwa maendeleo endelevu ya taifa hili’’.
Na,Daniel Manyanga
Mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) mkoa wa Simiyu imefanikiwa kukusanya kiasi cha fedha bilioni 14.2 kitokanacho kodi za walipakodi katika nusu ya mwaka wa fedha 2024/25 kati ya fedha bilioni 24.98 ambalo ni lengo katika mwaka huu wa fedha ambacho kimepangwa kukusanywa ili kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ya maendeleo hapa nchini.
Akizungumza katika hafra ya usiku wa shukrani kwa walipakodi ulioandaliwa na mamlaka ya mapato Tanzania(TRA) meneja wa mamlaka hiyo mkoa wa Simiyu, Joseph Mtandika amesema kuwa mkoa huo umeelekezwa kukusanya kiasi cha fedha bilioni 24.98 katika mwaka wa fedha 202425 lakini mpaka sasa wamefanikiwa kukusanya zaidi ya bilioni 14 kwa kipindi cha miezi sita kutoka Julai hadi Desemba mwaka jana.
Kenan Kihongosi ni mkuu wa mkoa wa Simiyu akizungumza katika hafra ya usiku wa shukrani kwa walipakodi amewataka walipakodi mkoani hapo kuhakikisha wanatimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari pasipo kusubiri kushurutishwa na mamlaka husika za kikodi kwani kodi hizo husaidia kuchochea shughuli za maendeleo ikiwemo kutekeleza miradi mbalimbali ya kimkakati hapa nchini.
Joseph Goryo,Jackson Samuel ni baadhi ya walipakodi waliopata tuzo za ulipakodi bora kwa hiari katika hafra hiyo wameeleza namna ambavyo tuzo hizo zitaleta chachu ya ushindani kwa walipakodi huku mwakilishi wa mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoa wa Simiyu,Boaz Ogolla ameishukuru mamalaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Simiyu kwa tuzo hizo hali ambayo inatambua umuhimu wa wafanyabiashara mkoani hapo.