

20 March 2025, 6:03 pm
Serikali kupitia Wizara ya Maji imeendea na adhima yake ya kuhakikisha inamtua mwanamke ndoo kichwani kwakuhakikisha inasogeza kuduma ya maji kwa wananchi.
Na,Alex Sayi-Maswa Simiyu
Wananchi na wakazi wa kijiji cha Ipililo kata ya Ipililo wilayani Maswa Mkoani Simiyu wameishukuru Serikali kwakuwasogezea huduma ya maji safi na salama.
Akizungumza na Sibuka fm wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa maji kijijini hapo Machi 19/2025 Diwani wa viti maalum Modesta Kabeya amesema kuwa wanaishukuru Serikali kwakuwajali wakazi hao.
Pelusi Goleka mkazi wa kijiji hicho amesema kuwa upatikanaji wa maji hayo utawaepusha wakazi hao kuepukana na magonjwa ya milipuko
Kwa upande wake Salumu Zefania ameishukuru Serikali kwa kukamirika kwa mradi huo wa maji safi na salama kijijini hapo
akisoma Taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Maji kijijini hapo Mhandisi (RUWASA)Jofrey Kiama amesema kuwa mradi huo tayari umeshakamirika kwa 90% na unatarajia kuwahudumia wakazi zaidi ya elf,9
Aidha kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Itilima Bi,Anna Gidalya akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Maswa amesema kuwa kukamirika kwa mradi huu kunatokana na juhudi za Mbuge wa Jimbo hilo Mh,Stanslaus Nyongo.