

19 February 2025, 8:30 pm
“Uongozi siyo kupiga kelele ni kuleta mabadiliko chanya katika eneo lako la kiutawala kama kuna changamoto zozote zile kwa wananchi tuanataka utuambie umefanya nini kuzitatua hizo shida ili jamii iseme kweli hapa tunakiongozi na siyo msindikizaji viongozi”.
Na, Daniel Manyanga
Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa Wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT)Taifa ndugu Mary Chatanda amewataka viongozi wanawake waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mwaka jana mkoani Simiyu kuwatumikia wananchi bila ubaguzi ukiwemo wa kivyama.
Mary Chatanda ametoa rai hiyo mapema leo hii kwenye mafunzo ya uhamasishaji wa matumizi ya matokeo ya sensa ya mwaka 2022 kwa viongozi wanawake waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa katika kuleta usawa wa maendeleo kwenye maeneo husika kulingana na ukubwa wa eneo ,uhitaji wa eneo na ongezeko la watu.
Akimwakilisha mtakwimu mkuu wa serikali Benedict Mugambi amesema mafunzo hayo yawasaidie viongozi hao kushiriki kikamilifu kwenye miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao ikiwemo na kukemea maswala ya rushwa.
Limi Silanga na Veronica Mabesa ni baadhi ya viongozi wanawake wa serikali za mtaa mkoani hapo wamesema kuwa mafunzo yatasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo ya kiutawala Ili kuleta usawa kwa wananchi.