

16 February 2025, 10:52 pm
Na Nicholaus Machunda
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM ) Mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali imejiimarisha katika kuinua zao la pamba ili kuleta tija kwa wakulima.
Mhe. Majaliwa amesema hayo wakati akihutubia wananchi wa Jimbo la Maswa Mashariki wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025 iliyofanyika katika uwanja wa Nguzo Nane uliopo mjini Maswa
Aidha amesema kuwa lengo la Chama Cha Mapinduzi na serikali ni kujikita kuboresha huduma za afya ili upunguza gharama za matibabu kwa wananchi ikiwemo wananchi wa wilaya ya Maswa.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2020/ 2025 Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki Mhe Stanslaus Nyongo amesema kuwa fedha nyingi zimetolewa na serikali kwa ajili ya maendeleo katika miradi ya maji, viwanda, afya, elimu, kilimo na ufugaji
Shemsa Mohamed ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Simiyu amewaomba wananchi wa Wilaya ya Maswa kumpa Rais zawadi ya kura nyingi za ushindi katika Uchaguzi Mkuu utaokaofanyika Oktoba mwaka huu.