

4 February 2025, 12:00 pm
Wananchi wanapaswa Kujifunza na kuelewa haki zao za Kisheria ili waweze kushiriki kikamilifu katika Mchakato wa haki na Dira ya Maendeleo hii itajenga Uwajibikaji kwa taasisi na wadau wa kutoka Haki -“Mhe Martha Mahumbuga”
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu Mh, Martha Johnbull Mahumbuga ametoa wito kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kujifunza haki zao za msingi ili waweze kushiriki kikamilifu katika mchakato wa haki na maendeleo.
Wito huo umetolewa feb, 03 2025 wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya sheria iliyofanyika katika viwanja vya mahakama hiyo wilayani bariadi mkoani simiyu.
Akitoa salamu za Serikali Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mh, Saimon Simalenga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh, Kenani Kihongosi amewapongeza kwa kufanya jukumu lao vizuri ,huku akiitaka Mahakama na wadau kuendelea kutoa elimu ili kuendelea kutambua haki zao.
Kwa upande wake mwendesha mashtaka wa serikali mkoa wa simiyu Mh, Anesius Kainunura amesema mahakama ndio chombo pekee cha utoaji wa haki, na kuongeza kuwa ili malengo makuu ya dira ya taifa ya maendeleo 2050 yaweze kufikiwa kama kila raia atapata haki yake ya msingi bila kikwazo.
Kwa upande wao wananchi wamesema kuwa wamependezwa nakuona kuwa uhuru wa mahakama upo lakini kuomba elimu izidi kutoolewa kwa wanawake na watoto hasa maeneo ya vijijini ambako wengi hawana elimu ya sheria.
Kauli mbiu katika Maadhimidho hayo ya wiki ya Sheria kwa Mwaka huu 2025 ni Tanzania ya 2050 nafasi za Taasisi zinazosimamia Haki madai katika kufikia malengo makuu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo.