WANANCHI WILAYANI MASWA WAASWA KUTUNZA VYANZO VYA MAJI.
27 July 2022, 11:41 am
Balozi wa Maji nchini Mrisho Mpoto maarufu kwa Jina la Mjomba Amewaasa Wananchi Wilayani Maswa Mkoani Simiyu kutunza vyanzo vya Maji likiwemo Bwawa la New Sola lililopo katika kijiji cha Zanzui kata ya Zanzui..
Balozi Mpoto ametoa nasaha hizo alipotembelea Bwawa hilo ili kijionea Uhifadhi wa chanzo hicho kinachohudumia Wananchi wa Mji wa Maswa na Vijiji 12 vinavyozunguka Bwawa hilo..
Amesema kuwa vyanzo vya Maji vilivyopo katika maeneo yetu ni Muhimu kwani vimekuwepo miaka mingi na kutunzwa na watu mbalimbali hadi kufikia hapa hivyo kila mwananchi anapaswa kuendelea kuvilinda na kuvitunza ili viweze kusaidia Jamii na Vizazi vijavyo..
“tutakapoingiza mifugo pale Ile mifugo itakwenda itakanyagakanyaka na ule udongo utalainika na kusababisha kina cha maji kupungua na tukiwa na mifugo mingi tukisema washambulie pale hatukai hata miezi sita maji yote yataisha lakini mifugo ile nyie mnajua tunaipeleka kwenye majosho inapigwa dawa na ng’ombe anywi maji ya mwanzoni anakunywa maji ya katikati akisogea pale ni kama anaoga na dawa yote inaishia kwenye maji… lakini hawa ng’ombe pia ninyi mnafahamu wanaweza kujisaidia pale kwahiyo maji yale yatachafuka na hivyo kuleta gharama kubwa ya kuyasafisha/ kuyatibu …lakini ng’ombe hao wanapoenda kunywa maji wanatengeneza njia na hivyo kusababisha maji kutoka na kupoteza muelekeo kwa hiyo hiki chanzo hakitakiwepo lakini ninyi mkaelilishana mkazungumza mkaona kwamba tunahitaji kukihifadhi hiki chanzo kiweze kutusaidia tena na tena niwapongeze sana ” amesema balozi Mpoto.
Aidha Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Victoria Dr Renatus Shinhu amesema kuwa ni vyema wakashirikiana na Wananchi wa Maeneo yanayozunguka Bwawa hilo katika Utunzaji , Utambuzi wa maeneo na Uwekaji wa Vigingi vya Mipaka.
Dr Shinhu amesema kuwa Bwawa hilo ni Muhimu kwani linategemewa na Wananchi wengi wa Mji wa Maswa hivyo ni Vizuri kuheshimu mipaka yote iliyowekwa kuzunguka Chanzo hicho ili kuepuka Uchafuzi wa Mazingira unaosababisha kukauka kwa Bwawa hilo..
Nandi Mathias ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Maswa-MAUWASA amesema kuwa Mradi huo umepunguza Magonjwa ya Matumbo na Kuhara hivyo wananchi kujikita katika Uazilishaji na kujiongezea Kiapato..
Nandi Mathias amesema kwa sasa Ushirikiano Umeongezeka kati ya Mauwasa na Wananchi wanaozunguka Chanzo hicho cha Maji hali inayopelekea Wananchi kuwa Sehemu ya Ulinzi wa Bwawa hilo..
Mbuke John ni mkazi wa kijiji cha Zanzui amesema bwawa hilo limekuwa msaada kwa wananchi kupata maji safi na salama huku mwenyekiti wa kijiji cha Mwabayanda Cosmas Kija akiomba ushirikishwaji wa wafugaji katika utunzaji uendelee sambamba na kufanya tathimini kutokana na idadi ya watumiaji kuongezeka .