

2 March 2025, 6:38 pm
Jamii Wilayani Maswa Mkoani Simiyu imeaswa kujenga tabia ya kuwatembelea wajawazito na wazazi wanaojifungua ili kusaidia mahitaji muhimu ya uzazi kwa wazazi hao.
Na,Alex Sayi Maswa-Simiyu
Uongozi wa Hospitali ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu umebainisha kuwa ndani ya mwezi mmoja hupokea wasitani wa kinamama wajawazito (400-450)
Hayo yamesemwa na mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo,Dr,Deogratius Mtaki, wakati akipokea baadhi ya zawadi zilizotolewa na umoja wa wanawake Wilayani Maswa Mkoani hapa kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Machi,08/2025.
kwa upande wake Afisa Maendeleo Wilaya na Mratibu wa dawati la jinsia Wilayani Maswa Mkoani hapa Bi,Basila Bruno amesema kuwa katika kuenzi siku ya wanawake Duniani kinamama hao kwa umoja wao wameamua kushiriki kufanya matendo ya huruma Hospitalini hapo.
Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa wanawake Wilayani Maswa Mkoani hapa na mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo Wilaya ya Maswa Bi,Caroline Shayo amesema kuwa wamefika Hospitalini hapo kutoa zawadi hiyo kidogo kwa watu wenye uhitaji.