Sibuka FM

Wafugaji Itilima watakiwa kutoingiza mifugo hifadhini

6 January 2025, 8:43 pm

Pichani ni mlezi wa chama cha wafugaji Tanzania, Joseph Makongolo akizungumza jambo na wafugaji hawapo kwenye picha Picha ni kitoka maktaba ya Sibuka fm

Mifugo inachangia pato la Taifa lakini hatuwezi kuacha maeneo ya hifadhi hapa nchini yaharibiwe na wafugaji wasiotaka kufuata sheria,kanuni na taratibu za uhifadhi katika kulinda uoto wa asili ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.” 

Na, Daniel Manyanga 

Wafugaji waishio pembezoni mwa maeneo ya hifadhi nchini wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa ikiwemo kutoingiza mifugo yao katika maeneo hayo kwa ajili ya malisho ili kuepuka kuingia kwenye migogoro na mamlaka za uhifadhi hali ambayo inapelekea baadhi ya wafugaji kutaifishwa kwa mifugo hao.

Kwenye picha ni mifugo ikiwa ifadhini katika moja wapo ya maeneo ya hifadhi picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

Rai hiyo imetolewa na mlezi wa chama cha wafugaji Tanzania (CCWT),Joseph Makongolo alipokutana na kuzungumza na wafugaji wa kata za Nkuyu,Ndolelezi,Chinamili,Mwaswale na Mhunze zilizopo wilayani Itilima mkoani Simiyu na kuwataka wafugaji kufuata Sheria zilizowekwa na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania katika kulinda hifadhi ili kuepuka kuwa sehemu ya migogoro na mamlaka za uhifadhi hapa nchini.

Sauti ya mlezi wa chama cha wafugaji nchini, Joseph Makongolo akiwataka wafugaji wilayani Itilima kufuata sheria za uhifadhi ili kuepuka migogoro

Samson Joseph,Ngwelu Kayanda,Yenga Bulengela na Malingo Kelebe ni baadhi ya wafugaji walioshiriki kikao hicho ambapo wametaja changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuiomba serikali izitafutie ufumbuzi wake.

Sauti za wafugaji wakizungumzia changamoto zinazowakabili katika ufugaji