2900 wapata huduma ya utengamao mkoani Simiyu
18 December 2024, 9:07 pm
“Kupatikana kwa huduma ya utengamao katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu kumepunguza gharama na muda kwa wananchi waliokuwa wanafuata huduma hiyo jijini Mwanza.”
Na, Daniel Manyanga
Zaidi ya wananchi 2900 mkoani Simiyu wamenufaika na huduma za utengamao kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa (Nyaumata)ambapo awali walilazimika kuzifuata huduma hiyo hospitali ya rufaa kanda ya ziwa (Bugando) jijini Mwanza ambapo walitumia gharama kubwa na muda mrefu
Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa huduma za tiba kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa Dkt.Juma Muna amesema kuwa tayari kwenye hospitali hiyo kuna karakana kwa ajili ya kutengeneza viungo tiba pamoja na huduma ya vifaa tiba saidizi.
Dkt.Hawa Otimong mkuu wa idara ya utengamao hospitali ya rufaa ya mkoa wa Simiyu amesema awali wagonjwa waliohitaji vifaa bandia walitakiwa kupewa rufaa ya kwenda hospitali ya rufaa kanda ya ziwa (Bugando) jijini Mwanza ambapo walitumia gharama kubwa na muda mrefu.
James Sitta na Happiness Juma ni baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamepatiwa huduma kwenye hospitali hiyo wamekiri watoto wao kuendelea vizuri kiafya.