Sibuka FM

TCB yagawa baiskeli 218 kwa wakulima wezeshi wa pamba Maswa

16 December 2024, 8:51 pm

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge akizungumza na wakulima wa Pamba wawezeshaji hawapo hapo pichani katika zoezi la ugawaji wa baiskeli Picha na Samwel Mwanga

Mkoa wa Simiyu ni mmoja wapo wa mkoa unaozalisha Pamba nyingi hapa nchini hivyo kuwa zao mkuu la kibiashara na lakimkakati zaidi.”

Na, Daniel Manyanga

Katika kuhakikisha kilimo cha zao la Pamba kinawatoa wakulima kimaisha bodi ya Pamba Tanzania (TCB) wilayani Maswa mkoani Simiyu imegawa baiskeli 218 kwa wakulima wawezeshaji ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwa kuendelea kutoa elimu ya kilimo bora na chenye tija.

Pichani ni wakulima wawezeshaji wakiwa nyuma ya baiskeli 218 zilizokabidhiwa kwao na bodi ya Pamba Tanzania

Akikabidhi baiskeli hizo kwa wakulima wawezeshaji mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge amesema kuwa  lengo la baiskeli hizo ni kurahisisha utendaji kazi na kuongeza uzalishaji wa Pamba ,kulima kwa tija ili kuongeza thamani ya zao hilo hasa kwa wakulima.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge akizungumza na wakulima wawezeshaji wakati wa kugawa vitendea kazi hivyo

Ally Mabruki ni mkaguzi wa bodi ya pamba wilaya ya Maswa amesema kuwa kukabidhi baiskeli hizo kwa wakulima wawezeshaji ni kuongeza uzalishaji na kulima kwa tija ili wakulima waweze kujikwamua na umasikini wa kipato.

Sauti ya Ally Mabruki mkaguzi wa bodi ya pamba wilaya ya Maswa akizungumza malengo ya baiskeli hizo kwa wakulima waliopata vitendea kazi.

Veronica Paul na Malita Sasa, ni baadhi ya wakulima wawezeshaji waliopata vitendea kazi hivyo wamesema kuwa watahakikisha wanafanya kazi iliyokusudia hasa kuleta thamani ya zao la Pamba kwa wakulima.

Sauti ya Veronica Paul,Malita Sasa wakielezea namna ambavyo wamefurahia ujio wa baiskeli hizo
Kwenye picha ni mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge akizungumza na wakulima wawezeshaji kabla ya kuanza kugawa baiskeli hizo Picha na Samwel Mwanga

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge amewataka wakulima wawezeshaji kuzitumia baiskeli hizo kwa malengo yaliyokusudiwa na bodi ya Pamba wilayani hapo na siyo vinginevyo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge akiwataka wakulima wawezeshaji waliopata vitendea kazi hivyo kuvitumia kwa malengo yaliyokusudiwa
Picha katika matukio mbalimbali zikionesha mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge akikabidhi baiskeli kwa wakulima wawezeshaji ili kuongeza uzalishaji wa zao la Pamba Picha na Samwel Mwanga