Maswa:Viongozi wanawake watumikieni wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao
10 December 2024, 11:37 am
“Uongozi ni dhamana ambayo umepewa na wananchi wenye imani na wewe hivyo ukipata nafasi jitahidi sana kuwa kioo kizuri kwenye jamii unayoiongoza ili siku moja uweze kukumbukwa kwa mazuri kutokana na utendaji kazi wako”.
Na, Daniel Manyanga
Wanawake viongozi walioshinda nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mnamo tarehe 27.November.2024 wilayani Maswa mkoani Simiyu wametakiwa kuwatumia wananchi pasipo kujali vyama vyao ,ukabila,hali zao za maisha na udini ili kuleta maendeleo katika maeneo wanayoongoza.
Wito huo umetolewa na kaimu katibu tawala wilaya ya Maswa , Emmanuel Saguda wakati wa hafra ya kuwapongeza wanawake hao waliothubutu kugombea nafasi mbalimbali na kushinda hafra iliyofanyika katika ukumbi mkubwa wa halmashauri hiyo.
Antonia Nkolela ni katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi CCM (UWT) wilaya ya Maswa amesema kuwa kiongozi ni kioo cha jamii hivyo amewataka wanawake hao kusimamia masilahi ya wananchi.
Awali akizungumza katika hafra hiyo mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Simiyu, Mwanahawa Saidi amesema kuwa lengo la hafra hiyo ni kuwapongeza wanawake viongozi kwa uthubutu wao wa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi mkoani hapo na kuibuka washindi.