NEC yawaomba wananchi Simiyu kujitokeza kuboresha taarifa zao
26 August 2024, 5:19 pm
Tume huru ya uchaguzi imewataka wananchi mkoani simiyu kujitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura, ili wawe na sifa za kushiriki uchaguzi ujao.
Akizungumza katika Mkutano huo uliowakutanisha wadau mbalimbali mhe. Jaji mustaafu MBAROUK S. MBAROUK amewataka wananchi Mkoani Simiyu wajitokeze katika zoezi hilo la uboreshaji wa taarifa zao.
Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa uchaguzi Bw Selemani Mutabora akatoa takwimu za idadi ya matarajio kwa walio na sifa za kujiandikisha katika Daftari za Wapiga simiyu ikikadiliwa kuwa wapiga kura wapya Zaidi ya laki 1.4 ikiwa ni ongezeko la Asilimis 16 ya Wapiga kura laki 9 walioandikishwa awamu iliyopita ya 2019/2020
Kwa upande wa Wadau walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na vyama vya siasa ambapo wamekili umuhimu wao katika kuhamasisha kupitia nafasi zao kama viongozi wa vyama mbalimbali.
Aidha katika uzinduzi huo Tume imezingatia makundi maalumu ikiwemo Watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali huku wakieleza changamoto za kimazingira katika maeneo na vituo vya kujiandishia.
Kumalizika kwa mkutano huo kunaashiria kuanza rasmi kwa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mzunguko wan ne kwa mikoa ya simiyu, mara na manyara kwa kaulimbiu ya ‘kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa kupata viongozi bora’ kajiandikishe sasa.