Sibuka FM

Shimo lakatisha maisha ya Anna, Martha Bariadi

19 July 2024, 2:27 pm

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga akitoa maelekezo ya kufanyika uchunguzi kubaini kiini cha tukio. Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

“Usalama wa maisha ni jambo muhimu ili kutimiza malengo ya wananchi wetu nchi bila kuhakikisha usalama wa maeneo wanapotoka wananchi hatuwezi kufikia azma ya maendeleo ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla”

Na Daniel Manyanga

Wanafunzi wawili waliotambulika kwa majina ya Anna Mayunga (14) na Martha Dickson (13) wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mahaha kata ya Bunamhala wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji lililopo kandokando ya barabara ambalo lilichimbwa kwa ajili ya kuchotea molam kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo baada ya kufika shuleni hapo na eneo la tukio na  kisha kutoa maelekezo ya uchunguzi kufanyika juu ya tukio hilo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Simon Simalenga akitoa maelekezo ya kufanyika kwa uchunguzi wa tukio hilo
Pichani ni muonekano wa dimbwi lililochukua maisha ya Anna na Martha. Picha na Daniel Manyanga

Charles Yamungu ni mmoja wa walimu wa shule ya msingi Mahaha ambaye anaeleza ni kwa namna gani watoto hao walitoka shuleni na kwenda katika dimbwi hilo.

Sauti ya mmoja ya walimu shuleni akizungumzia namna ambavyo wanafunzi hao walivyotoka darasani.

Kwa upande wao baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo na mmoja wa ndugu wa marehemu wameeleza tukio hilo lilivyotokea.

Sauti ya baadhi ya mashuhuda wa tukio wakizungumzia