RC Kihongosi aangiza Miradi ya RUWASA Simiyu Kukamilishwa kwa Wakati
4 July 2024, 10:37 am
Niwapongeze sana RUWASA Mkoa wa Simiyu kwa kazi kubwa mnayofanya ya kumheshimisha Mhe Rais Samia, kwakweli Sekta ya Maji imekuwa na Mageuzi makubwa sana, Niwaombe Mtekeleze miradi kwa Wakati na kwa Ubora ili Wananchi waweze kunufaika ” RC Kihongosi “
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe, Kenani Laban Kihongosi ameiagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini – RUWASA Mkoa wa Simiyu kuhakikisha Miradi wanayotekeleza kukamilika kwa Wakati na kwa Ubora ili iweze kunufaisha wananchi.
Mhe Kihongozi ametoa maagizo hayo katika kikao Kazi cha Mwaka cha RUWASA kilichofanyika Wilayani Busega na kusema kuwa Watanzania wanawategemea katika Upatikanaji wa Huduma ya Maji hivyo wana dhamana kubwa huku akizitaka taasisi zote za Serikali zinazodaiwa bili za Maji kulipa.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewapongeza Watumishi wa Ruwasa kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwahudumia wananchi katika Sekta ya Maji kwani kumekuwa na Mageuzi makubwa katika Sekta hiyo na kuendana na kauli ya Rais ya Kumtua Mama ndoo kichwani
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika Kikao kazi hicho, Kaimu Meneja wa RUWASA Mkoa wa Simiyu Mhandisi Emmanuel Luswetula amesema kuwa hadi kufika mwezi june mwaka huu 2024 Wastani wa upatikanaji wa huduma ya Maji umefikia Asilimia 70.
Mhandisi Lucas Madaha Meneja Ruwasa Wilaya ya Maswa, Mhandisi Nusra Msoke Kaimu Meneja Ruwasa Wilaya ya Bariadi na Mhandisi Daniel Gagala Meneja Ruwasa Wilaya ya Busega Wanaeleza namna wanavyotekeleza Miradi katika Wilaya na Mikakati yao ili kufikia Asilimia 76 ifikapo Desemba, 2024