DC Maswa awaasa madiwani kusimamia miradi ya Maendeleo inayotolewa na Serikali.
13 May 2021, 10:25 am
Mkuu wa wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Aswege Kaminyoge amewataka Madiwani kusimamia Miradi na kufuatilia maendeleo inayotolewa na Serikali katika maeneo yao..
Kauli hiyo ameitoa wakati akitoa Salamu za Serikali katika kikao cha Baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hapa Maswa.
Mh Kaminyoge amesema kuwa Diwani anapaswa kujua Fedha zote zinazoletwa kwenye kata yake na kufuatilia matumizi ya Fedha hizo..
Diwani wa viti maalumu kupitia Chama cha Mapinduzi Mh Pili Lameck amesema kuwa Madiwa wanauhusiano mzuri na Watendaji wa vijiji , kata na Halmashauri hivyo kuahidi kuendelea kutoa Ushirikiano.
Aidha Diwani wa kata ya Binza Ndugu Aroni Mboje ameiomba Serikali kutatua changamoto ya Mrundikano wa wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Maswa na kuhoji utaratibu wa waalimu kuhangaika na Madokezo badala ya kufanya kazi yao ya Kufundisha watoto..
Akijibu hoja hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa Dr Fredrick Sagamiko amesema kuwa wakuu wa Idara na wakuu wa Shule wataendelea kushirikiana na Kitengo cha Manunuzi cha halmashauri.