Mhe, BEREGE akabidhiwa Ofisi aahidi neema kwa wana Maswa
13 August 2021, 10:12 am
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Ndugu Saimoni Berege ameahidi kutoa ushirikiano kwa Madiwani na watumishi wa kada mbalimbali pamoja na kwakuendeleza miradi yote ambayo ilianzishwa na Mtangulizi wake Dr Fredrick Sagamiko ambaye kwa sasa amehamishiwa Manisipaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Hayo ameyasema wakati wa Makabidhiano ya Ofisi kati ya Mkurugenzi huyo mpya na Mkurugenzi ambaye aliyehamishiwa Manispaa ya Songea na kusema kuwa maendeleo yanaletwa kwa Ushirikiano wa Serikali na Wananchi..
Amesema kuwa yeye ataongoza kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu za Kiserikali hivyo Watumishi waache kufanya kazi kwa mazoea kwani yanazorotesha maendeleo ya wananchi.
Naye mwenyekiti wa Halmashuri ya Wilaya ya Maswa Mh, Paul Simoni Maige amesema kuwa mambo mengi amejifunza kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi Dr Sagamiko ambayo yanamsaidia katika kuongoza Halmashauri.
Aidha akikabidhi ofisi aliyekuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya hiyo Dr Fredrick Sagamiko amewashukuru Watumishi na wananchi wa wilaya ya Maswa kwa Ushirikiano waliompatia katika kutekeleza majukumu yake hivyo amekabidhi halmashauri kwa Mh Berege katika mikono Salama wananchi wasiwe na wasiwasi..
Hapa chini ni Picha mbalimbali za makabidhiano na maeneo waliyotembelea.