Sibuka FM

Halmashauri ya Wilaya  ya Maswa kutumia Bil  47.2 Mwaka wa Fedha  2025/2026

20 January 2025, 10:57 am

Pichani aliyesimama ni Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya ya Maswa Mhe Paul Maige wakati wa Baraza maalumu la Bajeti 2025/2026 Picha na Nicholaus Machunda

Bajeti hii imezingatia Miongozo na Sera mbalimbali pamoja na Vipaumbele Muhimu kwa wananchi wa Maswa “DED Maswa Ndugu Maisha Mtipa”

Baraza  la  Madiwani  katika  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  Mkoa   Simiyu  limepitisha  Bajeti  ya  Shilingi   Bilioni 47. 2  kwa  ajili  ya  Matumizi  kwa  mwaka  wa  Fedha  ujao  2025/2026  ikiwa  ni  Ongezeko  la  asilimia  0.81 % ya  Bajeti  ya  mwaka   2024/2025 ambayo  ilikuwa  Bilioni  46.8

Akiwasilisha   Rasimu ya  Mpango  wa   Bajeti   kwa  niaba  ya  Mkurugenzi  Mtendaji wa  Halmashauri   ya Wilaya  ya  Maswa,  Afisa  Mipango  wa  Halmashauri  hiyo  Ndugu  Julius  Ikongora  amesema  kuwa  Bajeti  hiyo  imekuwa  na  Ongezeko  kutokana  na  kuongezeka  kwa  Mapato  ya  ndani  ya  Halmashauri

Sauti ya Julius Ikongora Afisa Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Amesema  kuwa  katika  Makadirio  hayo  ya  Mpango  wa  Bajeti yamezingatia   Miongozo  na  Sera  mbalimbali   kama  vile  Dira  ya   Taifa, Malengo 17 ya  maendeleo  endelevu ya mwaka  2015-2035 pamoja na  maelekezo  ya  Viongozi  wa  Kitaifa, Chama  Tawala  na  Wizara.

Sauti ya Julius Ikongora Afisa Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Baada  ya  kuwasilishwa  kwa  Rasimu  ya  Bajeti  hiyo  baadhi  ya  Madiwani  katika  Halmashauri  hiyo Stephen   Dwese,  Esther  Ng’holongo  na  Bundala Isambaja   wakapata  nafasi ya  Kuchangia    na  kuwapongeza  waandaaji   kwani  imelenga   mambo  muhimu  ya  Wananchi  wa  Wilaya  ya Maswa.

Baadhi ya Madiwani walioshiriki kuchangia Rasimu ya Bajeti Halmashauri ya Maswa

Akitoa  ufafanuzi   wa  baadhi  ya  hoja  zilizoulizwa  na  Madiwani, Mkurugenzi  wa Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  Ndugu  Maisha  Mtipa  amesema  halmashauri  imejipanga  kuboresha  maeneo  hasa  eneo  la  Nh’ami  kunakojengwa  Viwanda  na   Jengo  la  Utawala   la  Halmashauri  hiyo.

Sauti ya Maisha Mtipa – Mkurugenzi Halmashauri ya Maswa
Picha: aliyesimama ni DED Maswa ndugu Maisha Mtipa akitoa Ufafanuzi wa Hoja za Madiwani

Baada  ya  majadiliano ya   Rasimu  ya  Bajeti  hiyo  Mwenyekiti  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  Mhe  Paul  Maige   akawahoji  Madiwani  na  kuipitisha  kuwa  Bajeti  rasmi  ya  mwaka  wa  Fedha 2025/2026.

Sauti ya Paul Maige Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa