Sibuka FM

Wananchi Maswa wawekeana mikakati kumaliza Ugonjwa wa Kipindupindu

15 January 2025, 1:50 pm

Picha ni Wananchi wa kata ya malampaka wakiwa wamepokea masinki ya vyoo vya kisasa kutoka kwa balozi wa kampeni ya Mtu ni afya Mrisho Mpoto Picha na Nicholaus Machunda

Kwakweli inashangaza sana kuona watu hadi karne hii hawana vyoo na badala yake wanaenda kujisaidia Vichakani. ” Mrisho Mpoto balozi wa kampeni ya Mtu ni afya

Wananchi  wa  kata  za  Sangamwalugesha,  Malampaka  na  Shanwa   zilizopo  Wilaya  ya  Maswa  Mkoa  wa  Simiyu   wameweka   mikakati  ya  kuhakikisha  wanatokomeza   Ugonjwa  wa  Kipindu pindu katika maneneo  yao

Wakizungumza  kwa  nyakati  tofauti  katika  Mikutano  ya  hadhara inayoratibiwa   na  Idara  ya  Afya  kupitia  kampeni  ya  “ Mtu  ni  afya”   chini  ya   Balozi  wa  ampeni  hiyo  Mrisho  Mpoto    wamesema  kuwa  kutokomeza  ugonjwa    wa   Kipindupindu  inawezekana

Sauti za wanachi kuhusu matumizi sahihi ya vyoo
Wananchi na wataalamu mbalimbali wakimsikiliza Mrisho Mpoto hayupo Pichani

Akitoa  taarifa  ya  hali  ya  vyoo  katika  kata  ya   Malampaka ,  Mtendaji  wa  kata  hiyo   Jiyahile  Gamaya  amesema  kuwa   jumla  ya  kaya  37  hazina   vyoo   hivyo  hupelekea  kwenda  kujisaidia  polini na  kuhatarisha  afya  za  watu  wengine

Sauti ya mtendaji kata ya Malampaka- Jiyahile Gamaya

Kwa upande  wake  mwenyekiti  wa  Kijiji   cha  Sangamwalugesha   ametoa  maagizo  kwa  wananchi  wake  hasa   kaya  ambazo  hazina  choo  kuhakikisha  wanachimba  na  wale  ambao  hawana  uwezo  wa  kuchimba   watasaidiwa  kupitia   wajumbe  wa  Serikali  yake  ya  kijiji.

Sauti ya mwenyekiti wa kijiji cha Sangamwalugesha

Mrisho  Mpoto  ni   Balozi  wa  kampeni  ya  Mtu  ni  afya  amesema  kuwa  wanapokosa  vyoo  na  kwenda kujisaidia  vichakani  wanachangia  kusambaa  kwa  Ugonjwa  wa  Kipindupindu

Sauti ya Mrisho Mpoto balozi wa Mtu ni afya

Aidha  Mpoto  ameeleza  hatua  tano  za  kuzingatia  katika  Unawaji  wa  Mikono   ili  kujikinga  na  Ugonjwa  wa  kipindu pindu

Sauti ya Mrisho Mpoto balozi wa kampeni ya mtu ni afya
Picha ni Mrisho Mpoto balozi wa kampeni ya Mtu ni afya akizungumza na Wananchi kuhusu namna ya kuzuia kipindupindu
Wananchi wa Malampaka wakifuatilia kampeni ya mtu ni afya -fanya kweli usibaki nyuma chini ya balozi Mrisho Mpoto